Jumanne, 22 Machi 2016
STARS YACHELEWESHA KESI YA KAZIMOTO
Kesi inayomkabili kiungo wa klabu ya Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mwinyi Kazimoto imeahirishwa hadi May 2 mwaka huu kutokana na nyota huyo kuwa kwenye majukumu ya kuitumikia timu ya taifa nchini Chad.
Kesi hiyo ambayo ilipangwa inasikilizwa mjini Shinyanga ilipangwa kusikilizwa March 21 imeahirishwa na hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Rahim Mushi mara baada ya kupokea barua ya udhuru kutoka kwa wakili wa mchezaji huyo Paul Kaunda.
Mushi amesema kutokana na kupokea barua hiyo hivyo imepangwa kusikilizwa May 2, 2016 kutokana na mchezaji huyo kuwa nje ya nchi akijiandaa na mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Chad kwenye michuano ya AFCON unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumatano.
Mwinyi Kazimoto anakabiliwa na kesi ya kudhuru mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Communications Mwanahiba Richard kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga February 10 mwaka huu kwa madai ya kumwandika vibaya October 10 mwaka jana mkoani Mbeya.
Kazimoto alipandishwa kizimbani February 22 mwaka huu na kusomewa mashtaka hayo na mwanasheria wa serikali Upendo Shemkole ambapo mtuhumiwa alikana mashtaka na kuomba apewe mwezi mmoja ili atafute wakili wa kumtetea na tayari amefanya hivyo.
KUNDI LA MWISHO LAKAMILISHA JESHI LA STARS CHAD
...
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimekamilika baada ya kundi la pili lenye wachezaji nane kuwasili leo mchana nchini Chad tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Kundi hilo la pili limewasili majira ya saa sita mchana (saa za Chad) likiongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais za ZFA, Ravia Idarus na kupokelewa na viongozi waliopo jijini N’Djamena.
Mara baada ya kuwasili D’jamena wachezaji walipata nafasi ya kupumzika hotelini kabla ya kuelekea mazoezini kufanya mazoezi ya pamoja kwa wachezaji wote, yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charles Mkwasa amekiongoza kikosi chake chenye jumla ya wachezaji 20 kufanya mazoezi mepesi saa 9 mchana katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.
Katika mazoezi ya leo wachezaji wa Taifa Stars walionekana kuwa na umakini
mkubwa katika kusikiliza maelekezo ya kocha Mkwasa, huku morali ya wachezaji ikiwa juu kuelekea kusaka pointi 3 muhimu katika mchezo huo.
Wachezaji waliopo Chad ni magolikipa Aishi Manula na Ally Mustafa, walinzi Shomari Kapombe, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, David Mwantika, Erasto Nyoni na Kelvin Yondani.
Viungo ni Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazmito, Mohamed Ibrahim, Farid Musa,
Deus Kaseke na Shiza Kichuya, huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco, Ibrahim Ajibu, Thomas Ulimwengu na nahodha Mbwana Samatta.
Mechi kati ya Chad dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa kesho Jumatano saa 9:30 (saa 11:30 kwa saa za Tanzania) katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya jijini N’Djamena, na utarushwa moja moja na kituo cha luninga cha Taifa cha Chad (Tele Chad).
Jumamosi, 19 Machi 2016
The Blues boss felt the decision to award his side a late penalty against West Ham was correct and praised his players' comeback at Upton Park
Hiddink: Chelsea penalty looked correct
Getty
0
0
Guus Hiddink shrugged off controversy surrounding the late penalty that earned Chelseaa 2-2 draw against West Ham on Saturday and thought the decision looked accurate.
West Ham counterpart Slaven Bilic had described the decision by referee Robert Madley as "unacceptable", claiming that Michail Antonio had impeded Ruben Loftus-Cheek outside the penalty area with one minute of the encounter left to go.
But Hiddink's verdict was the foul took place on the line of the 18-yard box and that the benefit of the doubt had rightly been given to Chelsea in a marginal decision, with Cesc Fabregas subsequently scoring from the spot.
"I think that the real, fair judgement can be done when you have a camera very straight on the line because from my side, with a blue shirt, then you see he was tripped when he was on the line and the line is part of the box so there is a different view," the Dutchman told Sky Sports.
"Loftus-Cheek was through, he was about to score - which was prevented. Even if it was out, it is the benefit of the doubt to the attacking team in this case.
"Fabregas scored both of Chelsea's goals, the first time he had netted a double in a Premier League game since December 2009.
The last-gasp leveller from 12 yards meant the Blues stay unbeaten in the league since Jose Mourinho's sacking in December, a run of 14 matches.
"We had to react because we conceded two goals that were rather sloppy," Hiddink added. "We reacted for 10 or 15 minutes before half-time, especially with the beautiful Cesc Fabregas free-kick.
"We were controlling the second half and dominating the game. We got caught on the counter, but it is a compliment to the team to react as they did and then we got the late equaliser.
"We have reacted very well since December. It is difficult to get in the Champions League positions but the team has to have the desire they showed today to make a very good season at the end.
"I always like to be a bit critical of ourselves. Of course we are unbeaten and that is okay but by Chelsea's standards we have had too many draws.
"I would have liked to have had a few more victories and less draws but we have shown character, including today."
Arsenal yailaza Everton
Arsenal ilijibu kuondolewa kwake katika kombe la vilabu bingwa Ulaya pamoja na lile la FA baada ya kuishinda Everton katika uwanja wao wa Goodison Park.
Danny Welbeck aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya kufunga katika dakika ya saba ya kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi kutoka kwa Sancheza na kumchenga goli kabla ya kufunga.
Katika dakika ya 42 Kijana Alexi Iwobi aliwafurahisha mashabiki wa Arsenal baada yankufunga bao lake la kwanza katika kilabu hiyo.
Matokeo hayo yanaiweka Arsenal pointi nane nyuma ya viongozi wa ligi Leicester City.
Ni ushindi wa kwanza wa Arsenal katika mechi nne za ligi ya Uingereza.
Everton ilishambulia mara mbili pekee katika lango la Arsenal.
TBC,NSSF na RAHCO wapata wakurugenzi wapya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.
Pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO). Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
source EATV
Mlipuko wawauwa watu 4 Uturuki
Gavana wa Istanbul, Uturuki, anasema watu wanne wameuwawa katika mripuko wa bomu kufuatia shambulio la kujitolea mhanga katikati ya mji.
Watu wengine kama 20 wamejeruhiwa.
Picha za televisheni zimeonesha magari ya kubeba wagonjwa, yakielekea eneo la mashambulio, ambalo sasa limetengwa na polisi.
Jumapili iliyopita, shambulio jengine lilifanywa katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, na kuuwa watu 37.
Chama cha waopiganaji wa KiKurd, TAK, kilisema kilihusika na shambulio hilo.
Alhamisi, 17 Machi 2016
Ripoti: Ushindi wa Trump ni hatari kwa dunia
Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia.
Shirika hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani.
Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema "ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic".
Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea.
Kuyumba kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa Bw Trump.
"Kufikia sasa, Bw Trump ametoa maelezo machache sana kuhusu sera zake, na huwa anabadilisha sana msimamo wake,” EIU wanasema kwenye ripoti yao ya utathmini wa hatari zinazokabili dunia.
Utathmini huo huangazia pia athari za jambo fulani na uwezekano wa jambo hilo kutokea.
.Al-Shabab wamtumia Trump wakitafuta wafuasi
.US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
.Adele:Trump hana idhini ya kutumia nyimbo kisiasa
EIU hutumia kipimo cha moja hadi 25, na Bw Trump ana alama 12, sawa na hatari ya "kuongezeka kwa ugaidi wa kijihadi kuathiri uchumi wa dunia”.
"Amekuwa na msimamo mkali sana dhidi ya biashara huria, pamoja na Nafta, na ameituhumu Uchina mara nyingi kuwa taifa linalofanyia mchezo sarafu,” EIU inasema.
Shirika hilo limeonya kuwa matamshi yake makali dhidi ya Mexico na Uchina hasa yanaweza kusababisha vita vya kibiashara.
Bw Trump amependekeza ua ujengwe kati ya Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji na pia ametetea kuuawa kwa jamaa za magaidi. Aidha, amependekeza kuvamiwa kwa Syria ili kuangamiza kundi la Islamic State.
EIU wanasema pendekezo msimamo wake kuhusu mzozo Mashariki ya Kati pamoja na pendekezo kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani vinaweza kutumiwa na makundi ya itikadi kali za Kiislamu kuwatafuta wafuasi zaidi.
dunia
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)