Jumanne, 22 Machi 2016

STARS YACHELEWESHA KESI YA KAZIMOTO



Kesi inayomkabili kiungo wa klabu ya Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mwinyi Kazimoto imeahirishwa hadi May 2 mwaka huu kutokana na nyota huyo kuwa kwenye majukumu ya kuitumikia timu ya taifa nchini Chad.

Kesi hiyo ambayo ilipangwa inasikilizwa mjini Shinyanga ilipangwa kusikilizwa March 21 imeahirishwa na hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Rahim Mushi mara baada ya kupokea barua ya udhuru kutoka kwa wakili wa mchezaji huyo Paul Kaunda.

Mushi amesema kutokana na kupokea barua hiyo hivyo imepangwa kusikilizwa May 2, 2016 kutokana na mchezaji huyo kuwa nje ya nchi akijiandaa na mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Chad kwenye michuano ya AFCON unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumatano.

Mwinyi Kazimoto anakabiliwa na kesi ya kudhuru mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Communications Mwanahiba Richard kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga February 10 mwaka huu kwa madai ya kumwandika vibaya October 10 mwaka jana mkoani Mbeya.

Kazimoto alipandishwa kizimbani February 22 mwaka huu na kusomewa mashtaka hayo na mwanasheria wa serikali Upendo Shemkole ambapo mtuhumiwa alikana mashtaka na kuomba apewe mwezi mmoja ili atafute wakili wa kumtetea na tayari amefanya hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni