Gavana wa Istanbul, Uturuki, anasema watu wanne wameuwawa katika mripuko wa bomu kufuatia shambulio la kujitolea mhanga katikati ya mji.
Watu wengine kama 20 wamejeruhiwa.
Picha za televisheni zimeonesha magari ya kubeba wagonjwa, yakielekea eneo la mashambulio, ambalo sasa limetengwa na polisi.
Jumapili iliyopita, shambulio jengine lilifanywa katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, na kuuwa watu 37.
Chama cha waopiganaji wa KiKurd, TAK, kilisema kilihusika na shambulio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni